Showing posts with label Ufugaji. Show all posts
Showing posts with label Ufugaji. Show all posts

Friday, April 29, 2016

Mashine za kutotolesha mayai (Incubators)


Incubators ni Mashine zinazo tumika kutotoreshea viuombe mbali mabali hasa Ndege.

AINA ZA INCUBATORS
  • Forced Air Incubator
  • Still Air Incubators


FORCED AIR INCUBATOR
Forced Air Incubators ni mashine yenye Feni kwa ajili ya kutawanya joto ndani ya incubators

STILL AIR INCUBATORS
Hii ni mashine siyo kuwa na fane 

IPI NZURI?
Inashauriwa kutumia/kununua Forced Air Incubators ndo bora kabisa na haiatakusmbua na hatahivyo kwa incubator kubwa karibia zote ni Fored air, na mara nyingi ndogo ndo still air

AINZA INCUBATOR KWENYE OPERATION
Manual
Automatic

MANUAL INCUBATORS
Hizi hutumia mikono katika kugeuuza mayai na katika maswala mengine kama kucontro joto na kazalika

AUTOMATIC INCUBATORS
Hizi hujiendesha kama Computer, kila kitu hufanywa automatically so kazi za manual hupunguza sana, Ukiwa na Incubnator Automatic na ikawa na sehemu ambayo inajiongeza maji automatically basi inaweza hata kata wiki bila kuchungulia mashine yako na ikawa inapiga kazi bila tatizo.


NI IPI NZURI?
Kwa kweli kwa maisha ya sasa inahitajika Automati Incubators ambayo haitahitaji wewe kuwepo mara kwa mara katika ku contro mashine, Ingawa kuna wakati Manual inahitajika kuliko Automatic na kuna wakati Automatic inahitajika kuliko manual
NB: Automatic nyingi zina manual, yaani kuna sehemu ya kushft kwenda manual, ila manual karibia zote hazina sehemu ya kushift kwenda automatic

ILA ZOTE ZINAFANYA KAZI KWA UFANISI SAWA, TOFAUTI MOJA NI AUTOMATIC NA NYINGINE NI MANUAL.

MAMBO MUHIMU SANA KWENYE INCUBATORS
  • Aina ya incubators
  • Model of operation
  • Manufacture
  • Nguvu inazo tumia
  • Altenative source of power

 MANUFACTURE
Incubator nyingi za nje ni nzuri sana, Kuna za Italy, Denmark, Uk, China, USA, India, South Africa Trukey na kazalika na bei zinatofautiana. Na utaona kwamba Incubator kama za Uk, South, USA, Italy ni very expensive compare na za kutoka China au India. Ila bei kutofautiana sana sio ishu na kama mnavyo jua China wao wna Policy yao kuhusu Internatinal Trade that is why.

Mashine nza Ndani ya Nchi nazo zipo nzuri na zipo zingine ni vimeo ila watengenezaji wanatakiwa kuwekeza zaidi kwenye Utafiti na si kujikita kwenye mauzo, inatakiwa kuboreshwa zaidi na zaidi ili ziwe na viwango vizuri

SOURCE OF ENERGY
Incubators karibia zote zinatumia Umeme kama source namba one na jua, makaa yam awe au gas kama source namba mbili, ingawa zipo za mafuta ya taa pia kama source No 1

ALTENATIVE SOURCE OF ENERGY
Kila aina ya mtengenezaji ana source yake ya altenative energy, zipo za Gas, zipo za umeme jua na zipo za mvuke wa maji na zipo za mafuta ya taa, na zipo za makaa yam awe.

ALTENATIVE SOURCE NZURI
  • Kwangu mimi Incubators ambazo altenative source of energy ni Mvuke wa maji nimetokea kuzipenda sana
  • Hapa umeme ukikatika unaunga pipe kwenye Mashine na unakuwa na birika special na unaiweka jikoni maji yanachemka na mvuke unapita hadi kwenye incubators, ni source nzuri sana, 
  •  Hata jua nayo ni source poa

ILA BADO SOURCE YA JUA AU GAS INAKUWA NI ALTENATIVE NZURI SANA.


MATATIZO YA INCUBATORS
Incubators nyingi zina shida moja kubwa sana, Incubators inaweza ikaharibika na wewe usiwe na habari kabisa na mpaka uje kushutuka ilisha haribu mayai yote na hilo ni tatizo kubwa sana

MFANO:
  • Heating tube zinaweza kufa na wewe usijue kabisa, na ukija shitikia ilisha haribu kila kitu
  • Humidity Tube inaweza kufa na wewe usijue na ukija shitukia ni balaa
  • Eggs turning inaweza kufa na usitambue hata siku mbili 
  • Humidity sensor na temperature sonsor zinaweza kufa na wewe usijue chochote
  • Na mara nyingi kinaweza kufeli kifaa kimoja za vingine viakendelea na kazi bila shida ila ikawa ndo kama hivyo, Mfano Mashine inaweza kuwa imekufa Humidity tube, na hapo inaweza endelea kufanya kazi na some time ni vigumu sana kugundua.
  •  Na tofauti na mitambo kama gari, Incunator inapo haribika huku ukiwa umeweka mayai ni balaa tupu, kama huna mashine nyingine ndo inakuwa imeharibu mayai yote.


KUKATIKA KWA UMEME
Endapo umeme utakatika na ukatumia Gas, au mafuta ya taa au makaa yam awe kama source nyingine ni lazima ugeuze mayai kwa mkono, na hapa tatizo liko kwamba ile mashine haiwezi kukubali kugeka ni lazima ubonyeze sehemu ya kubadilisha kutoka automatic kwenda manual. HAPA NDO HUWA KUNA KAZI PEVU 

Na Mwisho ni kuhusu uendeshaji wa Incubators, Mara nyingi uendeshaji nao ni tatizo kubwa nasa hasa kwenye seting joto na humidity, make seting lazima zitofautiane kulingana na maeneo au vipindi Fulani, Joto na wakati wa Baridi kari

Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Dominick Haule
Mtoa Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanachama na watu mbalimbali.
Mawasiliano: +255 767 111173

Sunday, April 10, 2016

Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko


Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).

Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.